veri...
~ ewe tu Dada ~
ingawa wengineo kanipa kisogo ---
'nishikwe na mawazo
'kweli wapo wengi vipenzi
ila wachache wa kunibarizi
hapa na pale, warembo, wazuri,
waenzi kuduwaza, wasanifu, wajanja,
waaminifu, mienendo bainifu, tabasamu rogi,
waadilifu, waneni tamanishi, wakadhalika.
nikidhani kama... wenye maneno asali
kama wangapi hivi?
ee... wenye marinda mapaja yaniue!
kama vile... hebu basi nione
(https://emojis.wiki/emoji-pics/facebook/bouquet-facebook.png)
ah! Mola ndoto ifike... farasi ziwe takwa!
ama kweli wapo mabinti watabasamu jua
sura dhahabu... sauti ngoma
vinywele maua... mivuto marashi
tabia malaika... vituko sanaa!
sijui. Sijui kweli wangapi.
hmm. Yupo mmoja namfahamu
ingawa nilimjua tu kifupi... pia kirefu
kimsingi, pia kitani. Akanipa nikampa
nje ndani, raha tele kanipa!
lile Babe La Sura ---
mwanadada ameundwa, da!
akivaa basi umbo ndo hilo,
akitabasamu sura ndo hio,
atembee mahaga ndo hayo,
aketi atege misuli mapaja nayo!
(https://images.emojiterra.com/google/android-10/128px/1f339.png)
anikumbusha tu Kleopatra ama Julieti
wano ngano za kale tuliwasoma Fasihini
'wachanganya Mafarao na Mapilato eti.
au labda Nefertiti ---
Malkia wa Akhenaton wa Misri ya enzi.
hmm. Lahau la!
mradi nilimjua 'Adam bin Malaika
nidai chengine kipi tena basi?
wangapi katunukiwa kama mimi!
si shinde kana 'ili ndoto wala deja vu
yunu tu mwili roho sina
u wangu moyo wazi juu
nimpate nipae zote sawa!
(https://emojis.wiki/emoji-pics/messenger/hibiscus-messenger.png)
vipi je, utakubali sasa?
ewe tu Dada...